loader
Mwigulu afafanua kuongezeka deni la Taifa

Mwigulu afafanua kuongezeka deni la Taifa

WAZIRI wa Fedha na  Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema suala la kuongezeka kwa deni la Taifa ndivyo ilivyo kwa nchi zenye miradi mikubwa ya maendeleo.

Amesema hayo alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Juni 24, 2022 mjini Dodoma, wakati akifanya majumuisho ya hotuba ya bajeti ya mwaka 2022/2023 bungeni mjini Dodoma.

Amesema nchi zote zinazotengeneza miradi mikubwa ya maendeleo haziwezi kukosa madeni.

“Tulivyokuwa hatuna mkakati wa kuunganisha nchi kwa barabara za lami deni lilikuwa chini ya dola bilioni 10, tukatengeneza deni kwa kuchukua mkopo kuunganisha mikoa.

“Tunapoenda kutengeneza miradi mikubwa ya maendeleo lazima utengeneze deni, hivyo ndivyo inavyokuwa,” amesema Waziri Mwigulu.

Amesema baadhi ya madeni ni ya awamu mbalimbali za uongozi kuanzia Awamu ya Kwanza hadi Awamu ya Sita.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8184413309d10d9eaa1d5210225fe199.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi