loader
Rais Samia anajua maisha ya Watanzania

Rais Samia anajua maisha ya Watanzania

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema vitu vilivyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika bejeti ya mwaka huu, inaonesha anafahamu maisha ya Watanzania.

Amesema hayo alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Juni 24, 2022 mjini Dodoma, wakati akifanya majumuisho ya hotuba ya bajeti ya mwaka 2022/2023 bungeni mjini Dodoma.

Waziri Nchemba amesema ni vizuri wabunge waipitishe kwa kishindo bajeti hiyo na wakirudi majimboni kwao wana kila sababu ya kuwaeleza wananchi kwa nini wamepitisha bajeti hiyo.

Amesema ni bajeti ambayo imegusa kila kitu, ipo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa masikini, imegusa kilimo, imelenga kutoa unafuu wa maisha hasa katika masuala ya mafuta ya kula, ngano, mafuta ya nishati na mbolea.

“Mtasema mmepitisha ili kuunga mkono kujenga barabara maeneo ambayo hayapitiki, mtasema mmepitisha kuunga mkono jitihada za Rais katika nishati,” amesema Waziri Mwigulu na kuongeza kuwa kwa namna bajeti hiyo ilivyo inaonesha namna Rais Samia anavyoyajua vizuri maisha ya Watanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7a4a67f894c2235316726e87d5315697.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi