loader
Diwani ‘aliyepotea’ arejea kikaoni

Diwani ‘aliyepotea’ arejea kikaoni

HATIMAYE Diwani wa Kata ya Kawe, Mutta Rwakatare ameonekana kwa mara ya kwanza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Manispaa ya Kinondoni,  tangu Meya wa Baraza hilo, Songoro Mnyonge alipotangaza kutoonekana katika vikao mbalimbali tangu Machi mwaka huu.

Mapema leo Juni 24, 2022, akitangaza kwa furaha na bashasha katika Baraza la Madiwani lililohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, Meya Songoro Mnyonge, amesema diwani huyo wa kata ya Kawe ameonekana kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza kutokuonekana kwake kwenye mabaraza yaliyopita.

" .... baadae leo jioni tutakuwa na Get Together' na madiwani wengine kufurahia kurejea kwake, tunaamini hatapotea tena," amesema Meya huyo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d21600c3f370114822195ce0f3011bae.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi