loader
Mitandao ya kijamii na vita rushwa ya ngono vyuoni

Mitandao ya kijamii na vita rushwa ya ngono vyuoni

UTAFITI mdogo uliofanywa na Chuo Cha Ustawi wa Jamiii, Dar es Salaam umebaini kuwa mitandao ya kijamii inaweza kusaidia mapambano ya ukatili wa rushwa ya ngono nyuoni.

Utafiti huo uliofanyika kwa miezi mitatu uliohusisha makundi manne ya watu nane Hadi 14 ulifanyika katika mitandao ya Facebook, Instagram, Twitter, tiktok na whatsapp.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wahadhiri waliofanya utafiti huo, Dk. Wiliam Manyama, amesema  wamefanya utafiti huo kutokana na madhara kuwa makubwa na kutafuta suluhu.

"Malengo yetu ni  kujua aina ya mitandao inayotumika, tumefata mitazamo ya wanafunzi kuhusu mitandao na pia tumechunguza changamoto ambazo wanazipata ili waweze kukabiliana na matukio ya ukatili,"ameeleza.

Amesema mbinu waliyotumia ni kuhoji mtu mmoja mmoja na  makundi mawili ya jinsia ya kike na mawili ya kiume yasiyozidi watu 12.

 "Tulifanya mahojiano ya kina kwa washiriki 14 wanafunzi wa taasisi ya ustawi wa jamii hapa Dar es Salaam na Usagara, Mwanga, Kilimanjaro,” amesema.

Dk Mnyama allmebainisha kuwa matokeo ya utafiti huo ni kubaini mitandao pendwa na yanapendwa kwa sababu ya ushirikiano wa watu wengi.

"Wanafunzi wanauelewa mkubwa wa mitandao hiyo na mitandao haiepukiki, hivyo elimu itolewe ya matumizi bora,” amesema.

Ameeleza kuwa mitazamo waliyobaini ni chanya na hasi, ambapo kwa upande wa chanya mitandao inasaidia kupashana habari, kwani pale mtu hawezi kukutana uso kwa uso anatoa taarifa na kupata ushauri ni rahisi kupata msaada.

"Kama ukitumia vizuri unaweza kuwa salama na ni rahisi kujisajili,"amesema.

Amesema lwa upande wa mtazamo hasi, wengine wanasema mitandao inachangia ukatili uendelee isipotumika vizuri, kwani wengine wanatoa taarifa na kuzomewa.

"Pamoja na kuwepo kwa hoja kinzani tunahitimisha kuwa mitandao ya kijamii ina nafasi kubwa sana, kwani watu wengi wanakutana, hivyo ni hoja zenye nguvu," amefafanua.

Changamoto zilizoanishwa ni ukosefu wa fedha za kujiunga na vifurushi na kutoa taarifa na kuzomewa.

"Utafiti unalenga kupanua mawazo kukabiliana na ukatili wa kingono, elimu ni kitu cha muhimu kwani bado kuna changamoto ya kujua cha kuweka, watu gani na wakati gani hivyo wanafunzi watumie vizuri mitandao ya kijamii huwapatia haraka suluhu," amesisitiza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3a0dfd9e37f8b85fb6abaae200d9f2d5.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Aveline Kitomary

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi