loader
Kituo cha afya Makongro kitahudumia wakazi wote

Kituo cha afya Makongro kitahudumia wakazi wote

KITUO cha afya kinachojengwa katika Kata ya Rabour, kijijini Makongro Halmashauri ya Rorya mkoani Mara, kikikamilika kitahudumia wakazi wa Tarafa ya Luo-imbo kama rufaa ya zahanati zote zilizo kwenye tarafa hiyo.

Hayo yameelezwa na Serikali ya Mkoa wa Mara, kupitia taarifa yake iliyotiwa saini na Kaimu Ofisa Habari wa Mkoa huo, Stephano Amoni, ikifafanua masuala mbalimbali yanayohusu mradi huo, ikiwamo vigezo vilivyozingatiwa katika kuchagua eneo husika.

“Eneo lina ukubwa wa zaidi ya ekari kumi, linakidhi mahitaji ya ujenzi wa majengo 12, wamiliki wamelitoa kwa halmashauri kwa hiari, limepitishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kupitia vikao halali kisheria na jiografia yake ni rafiki, linafikia kirahisi,” anasema Amon kupitia taarifa hiyo.

Ujenzi wa kituo hicho umefikia hatua ya lenta na amesema unaendelea huku Kijiji cha Uliyo, kilichopo ndani ya kata hiyo kikiwa kimepokea Sh milioni 50 kutoka Serikali Kuu, kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ambayo inatakiwa kuanza kutoa huduma mapema iwezekanavyo.

Kupitia taarifa hiyo, uongozi wa Mkoa huo umewaomba wananchi wa Rorya na kwingineko nchini, kupuuza aina yoyote ya upotoshaji juu ya ujenzi wa kituo hicho cha afya huku ukiahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kwa kuzingatia muda, ubora na thamani ya fedha.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/da82c5dc9bb5b237eef4ed1d1a5766ca.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Editha Majura, Musoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi