loader
TIRA: Namna mfumo mpya wa bima ‘Takaful’ unavyofanya kazi

TIRA: Namna mfumo mpya wa bima ‘Takaful’ unavyofanya kazi

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeandaa mwongozo wa utoaji wa huduma za bima nchini kwa njia ya ‘Takaful’ kwa lengo la kuwavuta wateja ambao walikuwa wanashindwa kutumia mifumo iliyopo kutokana na misingi ya Imani yao.

Akizungumza na HabariLEO katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’ yanayoendelea jijini Dar es Salaam Ijumaa, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Mashariki, Frank Fred Shangali amesema huduma hiyo ni mpya katika soko la bima hapa nchini japo unatumiaka zaidi Ulaya na Uarabuni.

“Kuanzia mwaka huu tutakuwa na miongozo uliotolewa na Mamlaka [TIRA] ambao utaendana na matakwa ya watumiaji,” Kaimu Meneja huyo ameeleza.

Kwa mujibu wa Sehemu ya 9.1.1 ya kitabu cha Miongozo ya utoaji wa huduma ya bima inasema:

“Mwendesha Takaful atasimamia na kuwekeza fedha kwa usahihi na kufuata misingi ya Sharia kama inavyotekelezwa kimataifa na kuidhinishwa na Bodi ya Sharia.”

Aidha, Mwongozo huo unaainisha kwamba mwendesha Takaful atapaswa kuwa na mfumo ‘thabiti’ wa kusimamia fedha za za huduma hiyo.

“Hivyo ni lazima kuhakikisha mfumo huo unaweza:- (a) Kutambua uwekezaji unaofanywa na mfumo husika (b) Kubainisha kwa usahihi na kuweka hesabu ya ugawaji faida ya uwekezaji zilizopatikana kwa washiriki binafsi wa Takaful na Mwendesha Takaful.”

Pamoja na kufuata utaratibu huo, anaeleza Kaimu Meneja huyo, haimaanishi ni huduma ajili ya wateja wanaoiamini taratibu za Sharia bali ni kuongeza watumiaji wa bima ambao walikuwa wanaona mfumo wa sasa ‘conventional’ kama ni utapeli au kamari.

Mbali na eneo hilo, mmwongozo mwingine ni ule wa kusimamia watoaji huduma mmoja mmoja na ule wa utoaji huduma ya bima kupitia kampuni za mawasiliano.

“Tumelegeza masharti kwa watoa huduma lengo likiwa ni kuongeza ajira pamoja na kusambaza huduma kwa wananchi,” ameeleza.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/31a4097bd74b3f031ef0528452ee7750.jpeg

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja, Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Sauli Giliard

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi