loader
Mwenyekiti EABC abainisha mikakati ya kukuza biashara EAC

Mwenyekiti EABC abainisha mikakati ya kukuza biashara EAC

BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limedhamiria kufanya kazi na sekta binafsi katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kuendesha mchakato wa ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia biashara na uwekezaji .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti mpya wa EABC,  Angelina Ngalula baada ya kukutana na wadau na wakuu wa taasisi mbalimbali na sekta binafsi  na kuahidi mambo makubwa ya kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati kibiashara.

Ili kufanikisha hili, EABC inafanya kazi na sekta za umma, taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wasomi, na Jumuiya ya wafanyabiashara ili kufungua fursa za kiuchumi...hivyo naomba ushirikiano wa kutosha kuhakikisha tunafikia malengo ambayo tumeyakusudia, amesema Ngalula.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa katika kipindi chake cha miaka miwili, mambo makuu aliyojipanga kuyatekeleza ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, kuboresha mazingira ya biashara na kuboresha ushindani wa kibiashara.

Angelina amesema uongozi uliopita umefanya mambo mengi vizuri chini ya Baraza hilo la EABC, lakini bado kuna kazi ambazo ziko mbele yao, hususani uwakilishi wa kibiashara wenye ufanisi katika mikutano ya ngazi ya juu ya maamuzi ya sera za EAC.

Mwenyekiti huyo amesema EAC ndiyo Jumuiya inayoongoza kwa uchumi wa kikanda barani Afrika na kama Mwenyekiti wa EABC pamoja na Bodi yake, atahakikisha ukuaji wa biashara huria.

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5bdf06c9784c207d5de098a58a7b6e90.PNG

Kiongozi wa Azimio la Umoja ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi