loader
Mgombea urais Kenya aahidi mafisadi kuuawa

Mgombea urais Kenya aahidi mafisadi kuuawa

MGOMBEA wa urais nchini Kenya kwa tiketi ya chama cha Roots, Profesa George Luchiri Wajackoyah amesema Kenya inatakiwa kiongozi mwenye uthubutu na ambaye hawezi kukumbatiwa na mafisadi.

Wajackoyah alisema jana wakati akiwa katika Stendi Kuu ya Mabasi Mjini Nairobi katika mkutano wa kampeni na kuongeza kuwa endapo atachaguliwa kuliongoza taifa hilo ataweka sheria itakayotekeleza hukumu ya kifo kwa mafisadi wote bila huruma.

Alisema inawezekana kulipa madeni yote wanayodaiwa kama taifa na kuitajirisha nchi hiyo kwa muda mfupi sana kwa kutumia kilimo cha bangi, ufugaji wa nyoka, kuuza nyama ya mbwa na fisi ndani na nje ya taifa hilo.

Mgombea huyo ambaye alisomea sheria kuhusu uhamiaji, alisema kilimo cha bangi ndio suluhisho kwa matatizo yote ya uchumi wa Kenya na kwamba kitatatua changamoto za kifedha kwa wakenya wote

Profesa Wajackoya vilevile ameendelea kuwaambia wakenya kwamba ufugaji wa nyoka wenye sumu una faida kubwa kifedha. Kulingana na ilani yake ya uchaguzi, sumu kutoka kwenye nyoka hao itasafirishwa hadi nchini China na kutengeneza dawa za kutibu magonjwa ambayo hajayaeleza.

“Kila nyoka mwenye sumu ataleta dola 6,000 au Sh za Kenya 600,000. Kila mkenya atapata dola 5,300 kwa kila nyoka anayeuzwa. Tutatumia ufugaji wa nyoka kugharamia bajeti ya sekta ya elimu nzima,” alisema Wajackoya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/be8fa1176f6a869ef2ba00a69fc6c7cb.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi