loader
John Makelele kuzikwa Moshi kesho

John Makelele kuzikwa Moshi kesho

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, John Makelele ‘Ziga Zag’  aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa ana umri wa miaka 61, anatarajiwa kuzikwa kesho Moshi, Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa mke wa marehemu Salome, Makelele ameacha watoto watano, ambao ni Happy (42), Esther (38), Jastaz (32), Francis (29) na Elizabeth (22).

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali, Salome alisema mazishi yatafanyika kesho Jumanne nyumbani kwao, kijiji cha Mtakuja Moshi mkoani Kilimanjaro.

Makelele ambaye pia aliichezea timu ya taifa, alihamishiwa Muhimbili kwa matibabu wiki iliyopita akitokea Arusha baada ya hali yake kubadilika nyumbani kwake Manyara, alipokuwa anaishi na familia yake kufuatia kustaafu kazi benki ya CRDB.

Enzi za uhai wake, Makelele atakumbukwa zaidi baada ya kufunga bao la pili dakika ya 58 akimchambua kipa Sahau Kambi, marehemu pia Julai 23, 1988, Simba iliposhinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga na kunusurika kushuka daraja.

Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Edward Chumila, ambaye pia ni marehemu katika dakika ya 21, wakati la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na Issa Athumani dakika ya 36.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4c6587b7b6d10ccb1109ee63f5b913a4.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi