loader
Mambo mazuri mradi wa maji Bahi

Mambo mazuri mradi wa maji Bahi

ZAIDI ya wananchi 17,000 maeneo ya Bahi mjini mkoani Dodoma, wanatarajia kunufaika kupitia mradi wa maji unaotekelezwa kwa fedha za Maendeleo ya Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Mradi huo unatarajia kuboresha upatikanaji maji katika mji wa Bahi kwa kuongeza lita 528,000 kwa siku sawa na ongezeko la asilimia 51.7 za lita 377,000 zinazozalishwa kwa siku.

Akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajati ilipotembelea mradi huo juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, alisema ongezeko hilo litafanya uzalishaji kufikia lita 905,000 kwa siku sawa na asilimia 88.7.

“Serikali kwa kutambua athari za ugonjwa wa UVIKO-19 imetenga fedha za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa mfumo wa maji safi eneo la Bahi.

“DUWASA ilipokea fedha Sh milioni 451.5 kutekeleza mradi huu na DUWASA kupitia makusanyo yake ya ndani tuliongeza Sh mil 67.4 na kufanya jumla ya gharama za kutekeleza mradi huo ni Sh milioni 515.1, ambazo zilitumika katika kazi mbalimbali za mradi,” alifafanua.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5cee5022d0a40cda842a51b1f3b27e1f.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi