loader
‘Shirikianeni na wanaozunguka hifadhi’

‘Shirikianeni na wanaozunguka hifadhi’

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka askari wa uhifadhi nchini kujenga uhusiano mzuri na jamii inayozunguka maeneo ya hifadhi wanazozisimamia.

Ameyasema hayo leo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi alipotembelea Shamba la Miti la West Kilimanjaro, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa majukumu na kusikiliza changamoto zinazowakabili askari uhifadhi, ili kuzipatia ufumbuzi.

“Jamii ikiwa haina uhusiano mzuri hata ninyi haya mashamba hamuwezi kuyaendeleza vizuri, kwa hiyo lazima muhakikishe mnajenga uhusiano mzuri,” amesema Masanja.

Amesema jamii inapokuwa hairidhishwi na utendaji kazi wa wahifadhi, kunakuwa na migongano kati ya wananchi na wahifadhi hao na kufanya wahifadhi kuchukiwa na wananchi.

 

Amewapongeza askari uhifadhi wa Shamba la Miti la West Kilimanjaro kwa kuendeleza uhusiano mzuri na jamii kwa kugawa miche, kutoa ajira na kugawa magogo ya kutengeneza samani.

Kuhusu changamoto ya moto katika mashamba, Masanja ameelekeza wahifadhi kwenye mashamba yote nchini kushirikiana na serikali za mitaa, ili wananchi wanapoanza kuandaa mashamba yao wapate taarifa mapema na kuwaelekeza namna bora ya kudhibiti moto, kwa lengo la kuukinga usisambae kuepuka hasara inayotokana na moto.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu Shamba la Miti West Kilimanjaro, Masawanga Ismail amesema kuwa shamba limeendelea kuwa na uhusiano mzuri na vijiji  na taasisi zinazolizunguka ambapo imekuwa msaada mkubwa hasa wakati wa matukio ya moto, upandaji wa miti na uhalifu ndani ya msitu.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/51bb2472060a4947b37ba1a37ee97906.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi