loader
Rehmtullah azungumzia tuzo aliyoshinda Ghana

Rehmtullah azungumzia tuzo aliyoshinda Ghana

MBUNIFU wa mavazi nchini, Ally Rehmtullah, amesema tuzo ya Mbunifu Bora wa Kiume 2022, aliyoshinda nchini Ghana ni ishara kwamba anakubalika nje ya mipaka.

Mbunifu huyo alishinda tuzo hiyo mwezi uliopita katika tamasha liitwalo Ghana Merit Award.

Akizungumza na Habari Leo jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea tuzo hiyo, amesema anafurahi kuona ulimwengu unafatilia kazi yake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri.

"Nina furaha kwa sababu malengo yangu ya kuonesha uwezo wangu duniani yanazidi kufanikiwa siku hadi siku, niwashukuru wandaaji wa tuzo hizi, niwaombe waendelee kuandaa kwa sababu inatupatia motisha ya kufanya kazi nzuri kila kukicha," amesema Rehmtullah.

Pia amesema ataendelea kufanya kazi yake kwa bidii na kuwasaidia wabunifu wengine, hususani wachanga ili kuibua vipaji vipya nchini.

Kwa upande wake mwakilishi wa tamasha hilo, Michael Lincoln, aliyekuja kukabidhi tuzo,  amesema Tanzania ni moja ya nchi inayofanya vizuri katika tasnia ya mitindo barani Afrika na wabunifu wake wanafanya kazi nzuri ndiyo sababu utaona tuzo zaidi ya mbili zimekuja Tanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/12fd1e8986c0646f12c6f09e0f635ff7.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi