loader
Vinara NBC Dodoma International Marathon kuvuna 65m/-

KIASI cha Shilingi milioni 65 kimetengwa kama zawaid kwa washindi 15 watakaoibuka vinara kwenye mbio za NBC Dodoma International Marathon zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbio hizo za Kimataifa zitakayofanyika siku ya Jumapili, Julai 31, 2022 jijini Dodoma zitakuwa za umbali wa Kilomita 42, Kilomita 21 na kilomita 10.

 huku dhumuni likiwa ni kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Akitangaza zawadi za washindi, Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond amesema kuwa maandalizi yamekamilika na kwamba zawadi zitakazotolewa zimelenga kutoa hamasa kwa wanariadha  hususani wale wa ndani.

Mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake ataondoka na kitita cha Sh8, 000,000 kila mmoja huku wa pili akijitwalia Sh4, 000,000 wa tatu    Sh2, 000,000 wa nne Sh1,500,000 huku wa tano akijitwalia Sh1,000,000.

“Kwa kuzingatia kuwa mcheza kwao hutunzwa, kwa Mtanzania ambaye atakuwa wa kwanza ‘Overall Winner’ atapata Shilingi milioni nane na ataongezewa Shilingi milioni 2, hiyo ataondoka na jumla ya Shilingi milioni 10,” alisema.

Kwa upande wa Kilomita 21, mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni nne ambapo Mtanzania atakayeshika nafasi hiyo kuongezewa Shilingi Milioni moja na kufanya jumla ya Shilingi 5,000,000.

Mshindi wa pili atapata Sh2, 000,000, wa tatu 1,500,000 wa nne 1,000,000 wakati wa tano atajitwalia Sh. 700,000.

Mbio za Kilomita 10 mshindi atajipatia Sh. 1,500,000 wa pili Sh. 1,000,000 wa tatu Sh. 700.000 wa nne Sh. 500,000 wakati wa tano atajishindia Sh. 300,000.

Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu alisema mbio za mwaka huu zimelenga katika kutoa elimu ya saratani ambapo wameshirikiana na taasisi ya Ocean Road ili kufanikisha zoezi hilo.

“Kikubwa kwenye zoezi hili ni kutengeneza utamaduni wa kupima mara kwa mara na sisi tunaamini kwa kutumia Marathon hii itatupa platform (jukwaa) kubwa zaidi na tunaamini tutawafikia watu wengi zaidi,” alisema.

Aliongeza kuwa mbio hizo zitasaidia katika kufungua mipaka ya kibiashara katika mambo mbalimbali ikiwamo zao la zabibu ambapo wawekezaji watapata fursa ya kujionea uzalishaji wake na namna gani wanavyoweza kushikrikiana na Serikali kwenye eneo hilo.

Vinara NBC Dodoma International Marathon kuvuna 65m/-

KIASI cha Shilingi milioni 65 kimetengwa kama zawaid kwa washindi 15 watakaoibuka vinara kwenye mbio za NBC Dodoma International Marathon zinazotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbio hizo za Kimataifa zitakayofanyika siku ya Jumapili, Julai 31, 2022 jijini Dodoma zitakuwa za umbali wa Kilomita 42, Kilomita 21 na kilomita 10.

 Dhumuni la mbio hizo ni kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Akitangaza zawadi za washindi, Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond amesema kuwa maandalizi yamekamilika na kwamba zawadi zitakazotolewa zimelenga kutoa hamasa kwa wanariadha  hususani wale wa ndani.

Mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake ataondoka na kitita cha Sh8, 000,000 kila mmoja huku wa pili akijitwalia Sh4, 000,000 wa tatu    Sh2, 000,000 wa nne Sh1,500,000 huku wa tano akijitwalia Sh1,000,000.

“Kwa kuzingatia kuwa mcheza kwao hutunzwa, kwa Mtanzania ambaye atakuwa wa kwanza ‘Overall Winner’ atapata Shilingi milioni nane na ataongezewa Shilingi milioni 2, hiyo ataondoka na jumla ya Shilingi milioni 10,” alisema.

Kwa upande wa Kilomita 21, mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni nne ambapo Mtanzania atakayeshika nafasi hiyo kuongezewa Shilingi Milioni moja na kufanya jumla ya Shilingi 5,000,000.

Mshindi wa pili atapata Sh2, 000,000, wa tatu 1,500,000 wa nne 1,000,000 wakati wa tano atajitwalia Sh. 700,000.

Mbio za Kilomita 10 mshindi atajipatia Sh. 1,500,000 wa pili Sh. 1,000,000 wa tatu Sh. 700.000 wa nne Sh. 500,000 wakati wa tano atajishindia Sh. 300,000.

Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu alisema mbio za mwaka huu zimelenga katika kutoa elimu ya saratani ambapo wameshirikiana na taasisi ya Ocean Road ili kufanikisha zoezi hilo.

“Kikubwa kwenye zoezi hili ni kutengeneza utamaduni wa kupima mara kwa mara na sisi tunaamini kwa kutumia Marathon hii itatupa platform (jukwaa) kubwa zaidi na tunaamini tutawafikia watu wengi zaidi,” alisema.

Aliongeza kuwa mbio hizo zitasaidia katika kufungua mipaka ya kibiashara katika mambo mbalimbali ikiwamo zao la zabibu ambapo wawekezaji watapata fursa ya kujionea uzalishaji wake na namna gani wanavyoweza kushikrikiana na Serikali kwenye eneo hilo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8020d0c4824818f6f2e2515f180be991.PNG

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi