loader
'Msigeuze pikipiki za kilimo kuwa bodaboda'

'Msigeuze pikipiki za kilimo kuwa bodaboda'

MKUU wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe amewataka maafisa ugani kutumia pikipiki 39 walizopewa na serikali kwa ajili ya kutatua changamoto za wakulima, badala ya kuzitumia kwa maslahi binafsi.

Mwaisumbe ametoa hadhari hiyo leo wakati wa ugawaji pikipiki hizo kwa maafisa ugani wa kata mbalimbali wilayani hapo.

Mwaisumbe ameasa kutumia pikipiki hizo kwa uzalishaji wenye tija, badala ya kuzigeuza kuwa za biashara (bodaboda).

Anasema pikipiki hizo ziendande na tija ya wizara ya kilimo chini ya Waziri wake, Hussein Bashe katika mkakati wa kuinua sekta ya kilimo kuwa ya biashara badala ya wakulima kutonufaika na kilimo hicho.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Raphael Siumbu amewataka maafisa hao kutumia vyema vyombo hivyo vya moto, ili kupeuka ajali wawapo kazini kwani vyombo hivyo ni vizuri, ila vikutumiwa vibaya vinaweza kuleta madhara kwao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/496cd3f349966245e96d0179ca5605d0.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Monduli

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi