loader
Hospitali Bugando yaboresha huduma za ICU

Hospitali Bugando yaboresha huduma za ICU

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, imefanikiwa kuboresha huduma za chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU, kwa kuweza kuongeza vifaa tiba pamoja na utanuzi wa majengo mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk. Fabian Masaga wakati wa uzinduzi.

‘’ Hospitali yetu ilitengewa jumla ya Sh bilioni 4.2 kupitia fedha za UVIKO 19 na mpaka sasa tumepokea Sh bilioni 3.9, ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati wa ICU pamoja na ununuzi wa vifaa tiba.

“Fedha nyingine zilizobakia Wizara ya Afya inakamilisha hatua za kutununulia gari la kubebea wagonjwa na gari malumu la kuhifadhia na kusafirisha damu,’’ amesema Dk Masaga.

Amesema upanuzi wa ICU umejumuisha upanuzi wa ICU ya wagonjwa wa ndani, magonjwa ya upasuaji na magonjwa ya watoto wachanga.

‘’Kabla ya maboresho haya tulikuwa na ICU yenye vitanda 12 kwa magonjwa ya ndani na upasuaji pamoja na vitanda 12 kwa watoto wachanga,’’ amesema Dk Masaga.

Amesema baada ya maboresho, kwa sasa ICU yao ina uwezo wa jumla ya vitanda 51, ambapo magonjwa ya ndani kuna vitanda 11, magonjwa ya upasuaji kuna vitanda 19 na magonjwa ya watoto kuna vitanda 21.

Amesema kabla ya maboresho ICU yao ilikuwa na uwezo wa kubeba wagonjwa 21 na sasa baada ya maboresho inaweza kuhudumia wagonjwa 51.

Naye Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika mipango yake ya kuboresha huduma ya afya nchini.

Pia ameipongeza hospitali hiy kwa kuweza kukamilisha maboresho ya mradi huo wa ICU kwa wakati.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/024a06aa00d9c300403361549ff5bf98.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi