loader
Fursa kufundisha Kiswahili Afrika Kusini yaiva

Fursa kufundisha Kiswahili Afrika Kusini yaiva

SERIKALI imetangaza fursa ya walimu kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini na watakaochaguliwa ni wenye kujua kwa ufasaha lugha hiyo na Kiingereza.

Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, alisema hayo jana Dar es Salam katika maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya Kiswahili duniani yatakayofanyika Julai 7 mwaka huu.

Amesema katika kuhakiksha Kiswahili kinakuzwa maeneo mbalimballi, Tanzania na Afrika Kusini watasaini mkataba wa makubaliano ya ufundishaji  wa lugha hiyo nchini humo.

Tayari Waziri wa elimu wa Afrika Kusini, yupo nchini akiongozana na wajumbe mbalimbali kwa ajili ya tukio hilo.

Amesema walimu watakaochaguliwa ni muhimu kuzijua kwa ufasaha lugha hizo na sio wasiojua au kuchanganya herufi katika ufundishaji.

" Kuna watu wenye tatizo la herufi kama L na R, ambapo hao watakuwa wapotoshaji wa Kiswahili," amesema Mkenda na kuongeza kuwa  kiswahili ni lugha muhimu kwa fursa mbalimbali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/090cbbce39cfabc46aeac756ad8a9546.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi