loader
MSCL yafafanua nauli Mv Victoria, Butiama

MSCL yafafanua nauli Mv Victoria, Butiama

Kufuatia malalamiko ya upandaji wa nauli meli za MV Victoria na MV Butiama kwamba umefanyika kiholela, Kampuni ya huduma za meli (MSCL), imesema taratibu zote zilifuatwa, ikiwemo kukutana na wamiliki wa vyombo vya majini na wananchi kwa ujumla.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa MSCL, Philemon Bagambilana, amefafanua leo Julai 5, 2022 kwamba mabadiliko ya nauli za usafiri wa vyombo vya maji yanadhibitiwa na kuratibiwa na Shirika la Uwakala wa Meli  nchini (TASAC), ambalo lilifanya kikao cha wadau kukusanya maoni, Mei 20 mwaka huu, jijini hapa.

  “Kuna wamiliki wa vyombo vya maji waliomba nauli ziongezeke kwa asilimia 100, kuna wananchi waliokubali nauli ipande walau kwa asilimia 50 na kuna wadau waliotaka vyombo vya usafiri wa maji vipewe ruzuku ili kukabiliana na hali ya gharama za uendeshaji kuwa juu,” amesema na kuongeza kwamba:

“ Baada ya kupokea maoni  na kuyachakata kwa kuzingatia vigezo vya kiuchumi na kijamii, TASAC ilikuja na ukomo wa nauli kwa Ziwa Victoria kuwa asilimia 32.5 kwa vyombo vikubwa na asilimia 21.4 kwa vyombo vidogo, kama ilivyotangazwa katika tangazo la serikali namba 457 la Juni 24, mwaka huu.”

Akijibu swali la kwa nini nauli kupanda, Bagambilana amesema ni kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, ikiwemo mafuta na vilainishi, ambavyo vinachangia zaidi ya asilimia 85 ya gharama zote za uendeshaji.

Nauli mpya zimeanza kutumika rasmi jana Julai 4, ambapo daraja la kwanza kwa MV Victoria imekua Sh 55,000 kutoka Sh 45,000, daraja la pili Sh 40,000 kutoka Sh 30,000 na daraja la tatu Sh 21,000 kutoka Sh 16,000.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2a78b47e387113feed7daf25c9431dfc.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Abela Msikula, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi