loader
Mradi wa kufufua umeme Rusumo wafikia patamu 

Mradi wa kufufua umeme Rusumo wafikia patamu 

MAKATIBU Wakuu Wizara ya Nishati na Wizara ya Fedha na Mipango wametembelea mradi wa kufua umeme unaondelea wilayani Ngara, eneo la Rusumo utokanao  na maji ya Mto Kagera na kuridhishwa na utekelezaji wake.

Mradi huo utazalisha megawatt 80 na kuhudumia nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi na kulizishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emanuel Tutumba amesema ameridhishwa namna ambavyo  fedha  zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza mradi huo, zinavyotumika kwa usahihi na kusema mradi umekamilika kwa asilimia 95. 

Amesema lengo la ziara yao ni kuangalia maelekezo wanayoyatoa katika kuratibu na kusimamia mradi huo, kama yanatekelezwa  na baada ya ukaguzi wameviambia vyombo vya habari kuwa mradi huo utakamilika kwa asilimia 100, ifikapo Novemba mwaka huu.

"Tumeridhika na mradi unavyotekelezwa, ingawa tunajua mradi huo ulipangwa kukamilika mwaka jana, lakini miradi ya kimataifa ina mambo mbalimbali na changamoto kutokana na watoa fedha wanavyokuwa wametoa masharti yao.

“Lakini Sasa tunaona changamoto zimefikia mwisho na mradi huo upo mwisho kabisa kwa asilimia 95 na fedha  zinazotolewa na serikali zinatumika vizuri sana, "alisema Tutumba.

Alisema miradi iliyopaswa kutekelezwa kwa jamii yenye thamani ya Sh Bilion 23 kwa awamu ya kwanza imekamilika na  awamu ya pili inaaanza kutekelezwa, ambapo Wilaya ya Ngara imepata vituo vya afya, maji katika vijiji viwili vilivyo karibu na mradi, vyoo shuleni, madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felichesm Mramba, alisema kuwa uwepo wa mradi huo utausaidia Mkoa wa Kagera kuingia katika  gridi ya Taifa pamoja na Mkoa wa Kigoma kupata umeme wa uhakika kupitia kituo cha Nyakanazi.

Alisema mpaka sasa Wizara ya Nishati, imefanya uhakiki wa malipo ya fidia kwa watu 1,400, ambao wamelipwa, huku akiomba Wizara ya Ardhi kuharakisha mchakato wa uhakiki kwa wananchi wanaoishi kandokando ya Mto Kagera, ambao wanapaswa kupisha mradi na kuacha uharibifu katika vyanzo vya maji.

Mambo makubwa yaliyokamilika katika mradi huo kwa sasa ni ujenzi wa bwawa, nyumba ya mitambo, sehemu ya kuwashia umeme, huku kazi ndogo  za asilimia 5 zilizobaki ni kuunganisha nyaya na kazi nyingine ndogondogo katika mradi, ili kila nchi iwezi kunufaika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7fb66f07773b4ccaebd403dfd0b7aa87.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Diana Deus, Ngara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi