loader
Majaliwa amshukuru Samia bil 54/- mradi wa maji

Majaliwa amshukuru Samia bil 54/- mradi wa maji

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imetoa Sh bilioni 54 kugharimia mradi wa maji wa Chiuwe utakaohudumia wilaya za Ruangwa na Nachingwea.

Majaliwa alisema hayo juzi jioni akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi katika vijiji vya Mchenganyumba, Mbecha na Chimbila ‘B’ akiwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Ruangwa.

Alisema maeneo mengi ya wilaya hiyo maji yake ni ya chumvi, hivyo serikali ilifanya utafiti na kubaini kuwa chanzo cha maji cha Chiuwe maji yake hayana chumvi na ni ya kutosha kuweza kuhudumia vijiji vya wilaya hiyo na wilaya jirani ya Nachingwea.

Majaliwa alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kuwezesha kutekelezwa kwa mradi huo.

Alitoa mwito kwa Watanzania kujiandaa kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa na viongozi kwenye maeneo wanayoishi.

Sensa ya watu na makazi imepangwa kufanyika nchini Agosti 23 mwaka huu. 

Akizungumzia mradi wa maji, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Ruangwa, Lawrence Mapunda alisema unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza itahusisha vijiji 34 vya Wilaya ya Ruangwa na 21 vya Wilaya ya Nachingwea.

Mapunda alisema ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, utakamilika mwaka 2025/2026.

“Kwa sasa utekelezaji wa mradi huu upo katika hatua ya manunuzi na unatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu kwa awamu zote,” alisema.

Mapunda alisema kukamilika kwa mradi huo kutamaliza tatizo la upatikanaji maji wilayani Ruangwa kwa zaidi ya asilimia 80. Chanzo cha maji cha Chiuwe kilichopo Nyangao kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 15 kwa siku huku mahitaji ya wilaya ya Ruangwa kwa siku ni tani milioni tisa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/da0298ae09dd914a07e9ee934486b74f.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi