loader
Sekondari za serikali, wasichana kiboko kidato cha 6

Sekondari za serikali, wasichana kiboko kidato cha 6

BARAZA la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita uliofanyika Mei 9-27, mwaka huu yakionesha watahiniwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Matokeo hayo yanaonesha wasichana waliofaulu ni 40,907 sawa na asilimia 99.51 ya waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo ya mitihani hiyo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mazizini Unguja jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Salum Amasi alisema wavulana waliofaulu ni 52,229 sawa na asilimia 98.55 ikilinganisha na mwaka 2021 ambao waliofaulu walikuwa 87,043 sawa na asilimia 99.06.

Alisema watahiniwa 83,877 wa shule sawa na asilimia 99.24 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 37,170 sawa na asilimia 99.34 na wavulana ni 46,707 sawa na asilimia 99.16.

Shule 10 bora

Amasi alizitaja shule 10 bora kitaifa zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo zikiongozwa na Kemebos ya mkoani Kagera ni Kisimiri ya Arusha, Shule ya Wavulana Tabora na Shule ya Wasichana Tabora.

Nyingine ni Ahmes ya Mkoa wa Pwani, Dareda ya Manyara, Nyaishozi ya Kagera, Mzumbe ya Morogoro, Mkindi ya Tanga na Ziba ya Tabora.

Alisema katika mchanganuo huo, shule saba za serikali zimeongoza kwa kufanya vizuri ikilinganishwa na shule za binafsi.

Wanafunzi 10 bora sayansi

Katika matokeo ya wanafunzi 10 bora kitaifa kwa masomo ya sayansi, wasichana saba wameongoza wakiongozwa na Catherine Mwakasege wa Shule ya St Marys ya Mazinde Juu, mkoani Tanga.

Wanaomfuatia ni Lucy Magashi kutoka Shule ya St Marys Mazinde Juu, Minael Simon Mgonja, Norah Eliaza Kidjout, Jennifer Martin Chuwa, Pauline Ildephonce Mabamba na Rachel Joachim.

Wanafunzi 10 bora biashara

Kwa watahiniwa 10 bora kitaifa katika masomo ya biashara, wasichana wameendelea kutamba kwa kushika nafasi tisa za juu.

Wasichana hao ni Esther Chama wa Shule ya Kemebos, Dorcas Chacha kutoka Arusha, Nasra Ali Omar kutoka Zanzibar Commercial na Gladness Roman Swai kutoka Canossa Dar es Salaam.

Wengine ni Gladys Octavian Amlima kutoka St Christian Girls, Asya Rashid Ally kutoka Shaaban Robert, Edna Emanuel Urio wa Weruweru, Tecla Mshote kutoka Tusiime na Aisha Hilonda kutoka Tambaza, Dar es Salaam.

Amasi alisema ufaulu kwa ujumla umepanda kwa asilimia 0.25 ikilinganishwa na mwaka jana ulikuwa asilimia 99.62 na mwaka huu ni asilimia 99.87.

Aidha, alisema ubora wa watahiniwa waliofaulu vizuri katika daraja la kwanza, pili na tatu umeongezeka kwa asilimia 1.31 ikilinganishwa na mwaka jana.

Amasi alisema ufaulu wa jumla na ubora wa ufaulu kwa wasichana kwa mwaka huu umezidi kidogo wa wavulana kwa asilimia 0.08 na 0.18 mtawalia.

Matokeo 15 yafutwa

Alisema Necta imefuta matokeo ya watahiniwa 15 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao wakiwemo 13 wa shule na watatu wa kujitegemea.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/73fb158c04626e182df85bbe690df5cd.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi