loader
Wajumbe Costech watembelea miradi Z’bar

Wajumbe Costech watembelea miradi Z’bar

WAJUMBE wa Bodi ya makamishina ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), wametembelea miradi mbalimbali ukiwemo wa utengenezaji wa nyenzo inayotokana na maganda ya miwa kwa ajili ya kusafishia majitaka yanayotoka hospitalini.

Taarifa inasema kuwa miradi iliyotembelewa ni ya utafiti na ubunifu Visiwani Zanzibar.

Mradi mwingine walioutembelea ni wa kuongeza thamani ya dawa za asili na kuhifadhi mimea tiba inayotumika kutibu magonjwa yasioambukiza Zanzibar.

Costech kupitia mfuko wa Taifa wa kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MTUSATE), imefadhili miradi hiyo.

Kupitia mfuko huo, Costech imewekeza kiasi cha Sh milioni 100 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI), ili kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.

Pia wajumbe hao walitembelea maabara za mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar na kupata maelezo kuhusu miradi hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d344bd0fc174a0f96e35203a71d46525.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi