MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Yanga, Suma Mwaitenda ameainisha vipaumbele vyake atakavyoanza navyo endapo wanachama wa Yanga watamchagua.
Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye uzinduzi wa kampeni zake leo makao makuu ya Yanga, Suma amabey ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, amesema kuna mambo mengi amedhamiria kuyafanya, lakini kubwa ni kulinda umoja wa wanachama na mashabiki.
Amesema yeye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi na atatumia uwezo wake kutafuta vyonzo vingi vya fedha, ili kustawisha uchumi na kulinda mali za klabu.
“Yanga tuna malengo makubwa kuanzia kwenye mchakato wetu wa mabadiliko na mambo mengine mengi kuyafanikisha hayo uchumi wa klabu unatakiwa kuwa imara.
“Zinahitajika fedha kwa ajili ya kuongeza ushindani na maboresho ya kikosi chetu kwenye usajili,” alisema Mwaitenda.
Pia amesema atairudisha klabu kwa wanachama na kuongeza hamasa ya kujisajili kwa kadi za kielektroniki.