loader
Mambo matano yaliyochangia Waziri Mkuu wa Uingereza kujiuzulu

Mambo matano yaliyochangia Waziri Mkuu wa Uingereza kujiuzulu

KARIBU miaka mitatu iliyopita Waziri Mkuu Boris Johnson aliongoza chama chake kupata ushindi mkubwa ambao haukuwahi kushuhudiwa tangu uchaguzi wa 1987. Hata hivyo Kiongozi huyo amebwaga manyanga kufuatia shinikizo kutoka nje na ndani ya chama chake.
-
Shirika la Utangazaji la BBC limeweka wazi mambo makuu matano ambayo ni Maneno ya Naibu Kiongozi wa Wabunge wa Conservative, Chris Picher ambaye alidai kuwa Boris alihudhuria sherehe binafsi huko London ambako “alikunywa sana” na “alijiaibisha.”
-
Sababu nyingine imetajwa kuwa ni Kashfa ya Partygate. Inafahamika kuwa Mwezi Aprili, Boris alipigwa faini kwa kuvunja sheria za kutotoka nje. Mwezi Juni 2020, Boris alishiriki halfa kwenye bustani ya Downing Street kipindi ambacho serikali yake ilikuwa imezuia watu kukutana kama sehemu ya mapambano dhidi ya UVIKO-19.
-
Kupanda kwa gharama za maisha na kodi ambapo mfumuko wa bei umeongezeka kwa kasi mwaka 2022 hadi kufikia wastani wa asilimia 9.1. Sababu hii sana sana inatajwa kuchangiwa na mgogoro wa Ukraine na Urusi ambapo Boris alifanya vikao mara kadhaa na Rais wa Ukraine huku akiahidi kuisaidia Ukraine.
-
Swala la Mbunge, Owen Paterson ambaye kamati ya Bunge la Commons ilipendekeza Oktoba 2021 kusimamishwa kwa siku 30 hata hivyo wabunge wa conservatives wakiongozwa na Boris walisimamisha mchakato huo. Peterson alivunja sheria za ushawishi, ili kujaribu kunufaisha kampuni zilizomlipa.

Boris Johnson alishinda kwa kura nyingi kutokana na sera iliyo wazi na rahisi kufuata ya - Get Brexit Done. Lakini tangu wakati huo, wakosoaji wake walisema, kulikuwa na ukosefu wa umakini na maoni huko Downing Street.
-
Mshauri wake wa zamani aligeuka kuwa mkosoaji mkuu, Dominic Cummings, alimshutumu mara kwa mara kuwa msururu wa manunuzi yaliyo nje ya udhibiti, akihama kutoka nafasi hadi nafasi.
-
Na kama mnavyofahamu Jana Habarileo ilichapisha habari kuhusu Waziri Mkuu Boris kukalia kuti kavu. Viongozi na Mawaziri kadhaa waliamua kujiuzulu nafasi zao na hadi jana karibu maofisa 38 walikuwa wameshaandika barua za kuachia ngazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/31bcf4d255f085e27ca52b08529d234f.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: LONDON

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi