loader
Waziri Mkuu wa zamani Japan auawa akihutubia

Waziri Mkuu wa zamani Japan auawa akihutubia

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi alipokuwa akihutubia kwenye kampeni za uchaguzi wa ubunge katika mji wa Nara nchini humo.

Abe (67) alipigwa risasi mara mbili, ambapo moja imempata kifuani na nyingine mgongoni iliysababisha aanguke chini.

Waziri Mkuu wa sasa wa nchi hiyo, Fumio Kishida alisema, mtuhumiwa alikamatwa baada ya tukio hilo.

Abe ambaye alikuwa Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani nchini Japan, alijiuzulu mwaka 2020 akitoa sababu za kiafya.

Alirithiwa na mshirika wake wa karibu Yoshihide Suga, ambaye baadaye nafasi yake ilichukuliwa na Fumio Kishida.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/57b251bafb29530c204fd59f5a2c302a.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Tokyo, Japan

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi