loader
CRDB yaandaa semina ya ujasiriamali kwa vijana

CRDB yaandaa semina ya ujasiriamali kwa vijana

Benki ya CRDB imetangaza kuandaa semina maalum iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua” kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii.

Akifafanua madhumuni ya malengo ya kuandaa semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko CRDB, Joseline Kamhanda amewaeleza wanahabari kuwa semina hiyo itakayofanyika 16 Julai, 2022 katika Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es Salaam iitatoa kutoa mafunzo ya namna bora ya kuendesha biashara kwa wajasiliamali wanaofanya biashara mtandao na kutoa elimu ya usimamizi wa fedha katika biashara.

Malengo mengine ni pamoja na elimu ya masoko ya fedha na mitaji, na namna bora za kuyaendea masoko hayo, elimu juu ya fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wajasiriamali nchini, pamoja na elimu ya urasimishaji wa biashara na faida zake kwa wajasiriamali.

Benki ya CRDB pia iliutumia mkutano huo na waandishi wa habari kuwashukuru washiriki wote wa maonesho, wafanyabiashara, taasisi, makampuni na wateja binafsi, ya sabasaba kwa kuendelea kuichagua benki hiyo kuwa mtoa huduma

Akitoa salamu hizo za shukrani, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Wadogo na Wakati Benki ya CRDB, Bonaventure Paul alisema msimu wa sabasaba wa mwaka huu umekuwa na mafanikio zaidi ambapo benki hiyo imeweza kuboresha huduma zake kwa wateja na kuweza kuwahudumia wateja wengi zaidi kupitia tawi maalum la benki lililopo katika viwanja vya sabasaba pamoja na CRDB Wakala.

 

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ce7702a83b9620a1365383dcad2bce79.JPG

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja, Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi