loader
Baba wa Oprah Winfrey afariki Dunia

Baba wa Oprah Winfrey afariki Dunia

BABA Mzazi wa Mwandishi, Mtayarishaji wa televisheni na Msanii Oprah Winfrey, Vernon Winfrey amefariki dunia siku chache tu baada ya Oprah kumuandalia hafla fupi ya kumshukuru na kuthamini mchango wa Vernon katika maisha yake.

Mzee Winfrey alikuwa na umri wa miaka 89. Oprah alithibitisha katika ukurasa wake wa Instagram kwamba baba yake alifariki Nashville, Tennessee, siku ya Ijumaa.

Julai 4, Oprah aliandaa hafla nyumbani kwa baba yake ambapo pia alimzawadia kiti cha kinyozi kuheshimu kazi ya baba yake ambaye alikuwa kinyozi na kumiliki duka lake huko Nashville kwa karibu miaka 50.

"Jana pamoja na familia iliyozunguka kando ya kitanda chake nilipata heshima takatifu ya kushuhudia mtu aliyehusika na maisha yangu, akivuta pumzi yake ya mwisho," mtu huyo maarufu kwenye tasnia ya vyombo vya habari na filamu aliandika. "Tuliweza kuhisi amani kuingia chumbani kwa kifo chake."

Vernon aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Jiji la Metro la Nashville kwa miaka 16 na alikuwa mdhamini wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Tennessee.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6920a7044e4a840203f8bb1e68b02810.jpeg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi