loader
Ugumu wa Maisha: Raia wavamia nyumbani kwa rais

Ugumu wa Maisha: Raia wavamia nyumbani kwa rais

RAIS na Waziri Mkuu wa Sri Lanka wamekubali kujiuzulu baada ya machafuko zaidi nchini humo katika miezi kadhaa ya maandamano ya kisiasa, huku waandamanaji wakivamia nyumba za maafisa wote wawili na kuchoma moto moja ya majengo kwa hasira kutokana na mzozo mkubwa wa kiuchumi wa taifa hilo.

Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe alisema ataondoka madarakani mara tu serikali mpya itakapowekwa, na saa chache baadaye Spika wa Bunge alisema Rais Gotabaya Rajapaksa atajiuzulu Jumatano. Shinikizo kwa viongozi wote wawili liliongezeka huku mdororo wa kiuchumi uliposababisha uhaba mkubwa wa vitu muhimu, na kuwaacha watu wakihangaika kununua chakula, mafuta na mahitaji mengine.

Polisi walikuwa wamejaribu kuzuia maandamano kwa amri ya kutotoka nje, hata hivyo, waliondoa zuio hilo huku mawakili na wanasiasa wa upinzani wakiyashutumu kuwa ni kinyume cha sheria. Maelfu ya waandamanaji waliingia katika mji mkuu, Colombo, na kuingia katika makazi yenye ngome ya Rajapaksa.

Picha za video zilionyesha umati wa watu wenye furaha wakimiminika kwenye kidimbwi cha bustani, wakiwa wamelala kwenye vitanda na kutumia kamera zao za rununu kunasa tukio hilo. Baadhi walitengeneza chai, huku wengine wakitoa taarifa kutoka kwenye chumba cha mikutano wakimtaka rais na waziri mkuu waondoke.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/94367d87da888e74010ee702291fc7b7.jpeg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Sri Lanka

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi