loader
Kampuni 3  kutoa huduma za bima kidijiti

Kampuni 3 kutoa huduma za bima kidijiti

MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) imetoa leseni kwa kampuni tatu zizizokidhi vigezo vya kutoa huduma za bima kidijiti. Kampuni hizo zilikabidhiwa leseni katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja ya Sabasaba.

Kamishna wa Bima wa TIRA, Dk Baghayo Saqware alizitaja kampuni hizo kuwa ni Vodacom kupitia Voda Bima, Axieva bima na IMATIC Tech. Dk Saqware alisema kampuni hizo zimekidhi vigezo vya kupewa leseni hizo na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kupata huduma za bima kwa njia ya kidijiti.

“Hata hapa sabasaba wananchi ni wengi wachangamkie huduma za bima kupitia kampuni hizi zinazotoa kwa njia ya kidigitali,hii inaongeza wigo wa huduma za bima na kwa urahisi zaidi,” alisema Dk Saqware. Alitumia fursa hiyo pia kuzitaka kampuni nyingine za bima zinazotoa huduma kidijiti zizingatie sheria ili zipate leseni ya kutoa huduma hizo.

Mkurugenzi wa M-pesa wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Epimark Mbeteni alisema leseni hiyo kwao ni hatua muhimu kwani wanahudumia zaidi ya wateja milioni 10. Alisema wana ushirika na kampuni za bima zaidi ya 12 ambazo wamekubaliana kusambaza huduma za bima kwa urahisi kwa wananchi kwa njia ya kidijiti.

“Kupitia vodabima tunatoa huduma za bima mbalimbali kama za afya na hii tunaifanya nchi nzima kidijiti, tunaishukuru TIRA na serikali kutupa miongozo ya kutoa huduma na hii inawasaidia watanzania wengi kupata huduma za bima kwa urahisi zaidi,” alisema Mbeteni.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/428a48ea5887be1b80a696e0ceaae521.jpeg

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja, Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Na Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi