loader
NBC yawalipa wakulima fidia kupitia Bima ya Mazao

NBC yawalipa wakulima fidia kupitia Bima ya Mazao

Kwa mara ya kwanza nchini, wakulima wa zao la tumbaku mkoani Tabora wamelipwa fidia na Benki ya NBC kufuatia hasara waliyoipata kutokana na uharibifu wa mazao yao baada ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika msimu uliopita.

Malipo ya fidia yamefanyika chini ya mpango wa Bima za Mazao wa Benki ya NBC.

Katika mpango huo, yyama vinne vya ushirika (AMCOS) vya Insolelansabo, Muloku, Ngulu Moja na Isenegezya vimepewa zaidi ya shilingi milioni tisa kwa lengo la kufidia hasara iliyosababishwa na kiwango cha juu cha mvua ambayo iuliharibu mazao.

Akizungumzwa wakati wa kukabidhi hundi ya fidia kwa vyama hivyo, Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke alisema fidia hiyo imetolewa kupitia mpango wa bima kwa wakulima ambayo inawalinda dhidi ya hasara zinazosababishwa na athari za hali ya hewa kama vile ukame, vimbunga, wadudu,mvua ya mawe na mengineyo.

Masuke alisema kuwa NBC inaamini kuwa kupitia mpango huo wa bima hiyo, vyama vitapunguza kwa kiwango kikubwa hasara zinazoweza kutokea kutokana mabadiliko ya hali ya hewa na majanga mengine yasiyotabirika na yaliyo nje ya uwezo wa mkulima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk.Batilda Buriani aliipongeza Benki ya NBC kwa kubuni huduma hiyo ambayo imetoa suluhisho juu ya majanga ambayo yamekuwa yakiwakumba wakulima kwa muda mrefu.

“Naipongeza sana Benki ya NBC kwa kuleta sokoni Bima hii ya mazao yenye lengo la kuwalinda wakulima pindi watapatapo majanga yanayoleta uharibifu wa mazao yao na hivyo kuwaletea hasara.

“Hakika bima hii ya kilimo itakuwa ni chachu kwa wakulima wetu wa zao la Tumbaku na wakulima wote nchini kuweza kulima bila kuwa na hofu juu ya majanga yeyote. Tunawashukuru sana Benki ya NBC kwa kuunga mkono adhma ya serikali yetu kwa kuja na huduma hii muhimu sana kwa wakulima wetu.

“Nawasihi sasa muongeze bima hii katika mazao mengine ya biashara na chakula ili kutoa ahueni kwa wakulima ambao ndio sekta kubwa na uti wa mgongo wa taifa letu,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/72bb45d4c8cdbe4fd824c4ed438cefed.PNG

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja, Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi