loader
Marekani yashtukia operesheni za China Indo-Pasifiki

Marekani yashtukia operesheni za China Indo-Pasifiki

OFISA Mkuu wa Jeshi la Marekani, Jenerali Mark Milley amesema Jeshi la China limekuwa hatari na la fujo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuwa tishio kwa Marekani na vikosi vingine washirika hususani eneo la Indo-Pasifiki.

Jenerali Milley ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vikosi vya Pamoja amesema idadi ya ndege na meli za China katika eneo hilo imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba kumekuwa na mwingiliano usio salama.

"Ujumbe ni kwamba Jeshi la China, angani na baharini, limekuwa na fujo zaidi na dhahiri zaidi katika eneo hili," Milley amesema na kuvitaka vikosi vya Marekani kukusanya maelezo juu ya mwingiliano kati ya Uchina, Marekani na washirika wengine katika eneo hilo.

Maoni yake yalikuja wakati Marekani inaongeza maradufu juhudi zake za kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya Pasifiki kama njia ya kukabiliana na China, ambayo inajaribu kupanua uwepo na ushawishi wake katika eneo hilo.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e801bb6839603b9401fbaad53989fa2d.jpeg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: US, Sunday

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi