loader
Tanzania: Mwongozo kwa biashara ya kubadili fedha kwa wanaoanza

Tanzania: Mwongozo kwa biashara ya kubadili fedha kwa wanaoanza

Katika kipindi cha miaka kadhaa sasa, Bara la Afrika limeshuhudia ukuaji mkubwa wa biashara ya rejareja ndogondogo na sheria kadhaa za soko zimekuwa zikitekelezwa katika nchi mbalimbali za Kiafrika.

Soko la fedha za kigeni barani Afrika limeshuhudia ukuaji wa kasi na makadirio ya sasa yanaonesha kuwa wafanyabiashara hai ni takribani milioni 1.3.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopo barani Afrika ambazo zinashuhudia kukua kwa umaarufi wa biashara rejareja ya kunadilisha fedha. Hata hivyo, kuna hatari na ugumu zinazowakabili wanaojihusisha na biashara hii.

Hapa, tunachambua mambo ambayo wafanyabiashara wanaoanza biashara hii nchini Tanzania kuzingatia ili waweze kufanikiwa.

1. Fungua akaunti na wakala aliyedhibitiwa

 Unapotafuta wakala wa fedha, ni muhimu kupata anasimamiwa na wakala anayetambulika kama vile Mamlaka ya Usimamizi wa Maadili ya Kifedha (FCA) au Tume ya masoko ya mitaji na dhamana (SEC), kwa mujibu wa www.forexbrokers.co.tz

Madalali na washauri wengi wasio waaminifu waliojaa mitaani watakuaminisha kuwa wanaweza kukusaidia ili upate fedha nyingi lakini lengo lao kuu ni kukutapeli.

Kwa hiyo, ikiwa una nia ya kufanya biashara hii, unapaswa kuanza kwa kutafuta wakala anayejulikana na kuhakikisha kuwa ameidhinishwa ipasavyo na mamlaka kuu za kiudhibiti.

2. Anza kufanya biashara na akaunti ya majaribio

Baada ya kukamilisha mchakato wa usajili na wakala wako unayemchagua, utakuwa na uwezo wa kutumia akaunti ya majaribio, ambayo itakuruhusu kufanya mazoezi ya kufanya biashara huku ukipata maelekezo ya uendeshaji wa soko na namna dhamani ya fedha inavyoweza kubadili.

Unaweza kupata ufahamu wa muundo wa soko na kuzifahamu huduma zote zinazotolewa na wakala unapofanya biashara kupitia akaunti ya majaribio.

Akaunti za majaribio huwapa wafanyabiashara wapya fursa muhimu ya kielimu kwa kuwasaidia kupata maarifa ya jinsi ya kukabiliana katika kupata ufahamu wa jinsi ya kukabiliana na mawimbi katika soko.  Fungua akaunti ya majaribio sasa

3. Fuatilia mwenendo wa soko

Hata wafanyabiashara wenye uzoefu zaidi hawana uhakika wa kufanikiwa kila wakati katika biashara zao. Kutokana na sababu hiyo, ni bora kuendelea kupata uelewa wa kila kinachojiri duniani kote ili uweze kufanya uabuzi sahihi wa kibiashara.

4. Mikakati ya utafiti biashara ya kubadili fedha (Forex)

Kuna njia kuu kadha wa kadha ambazo zinaweza kutumika wakati wa kufanya biashara ya kubadili fedha (Forex); kwa ufupi ni kuwa kila wakati wafanyabiashara huja na mbinu mpya. Wafanyabiashara makini watatumia mbinu mbalimbali na watafahamu kila moja inapaswa kutumika.

Uchambuzi wa kimsingi, unaojumuisha uchanganuzi wa mifumo ya kiuchumi na matukio ya habari au uchambuzi wa kiufundi utatengeneza mfumo wa biashara ya Forex (kuchanganua matukio ya kihitoria yahusuyo bei kupitia jedwali).

5. Tumia mbinu bora za kukabiliana na majanga

Ingawa amana ya chini inayohitajika na madalali wengi ni kati ya $100-$200 pekee, akaunti za biashara zinaweza kuanzishwa kwa kiasi kidogo cha dola za Kimarekani tano (5), takribani Sh12,000 pekee.

Swali kwa kwamba; ni kiasi gani cha fedha unapaswa kuweka kabla ya kuanza biashara? Kiasi gani unaweza kumudu kutumia na ni kiasi gani uko tayari kuchukua katika njia ya hatari kwenda kwenye mizania.

Wafanyabiashara wa kitaalamu wa Forex wanakubali kwamba mfanyabiashara haipaswi kuhatarisha zaidi ya asilimia 3 ya salio la akaunti zao.

 

 

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f31607044226924d7fa2f89acc560315.jpeg

KATIKA kipindi cha mwaka mmoja, Mamlaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi