loader
Taasisi 550 kushiriki Nane Nane Morogoro

Taasisi 550 kushiriki Nane Nane Morogoro

JUMLA ya Taasisi 552 zinatarajiwa kushiriki maonyesho ya Kanda ya Mashariki ya Nane nane yatakayofanyika katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere mkoani Morogoro kuanzia Julai 31 hadi Agosti 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kuwa maonyesho hayo ni ya 29 kwa Kanda hiyo ambapo yatazinduliwa rasmi Agosti 2.

Kunenge alisema kuwa maonyesho hayo ambayo kauli mbiu yake ni Ajenda ya kumi ya thelathini Kilimo ni biashara Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo Mifugo na Uvuvi itahusisha Wilaya 27 zenye Halmashauri 34.

"Kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzangu ninawakaribisha kushiriki kwenye maonyesho haya ya Nane nane Kanda ya Mashariki ambapo kutakuwa na Teknolojia mbalimbali za kilimo Mifugo na Uvuvi na burudani,"alisema Kunenge.

Alisema kuwa Taasisi 372 zimethibitisha kushiriki na zimekamilisha taratibu zote pamoja na maandalizi ya mabanda.

Aidha Kanda hiyo inaundwa na mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na wenyeji Morogoro.
 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6c133d3fa0dbce768a082dd6952ca6c1.jpeg

UKOSEFU wa elimu ya biashara, uthubutu na ...

foto
Mwandishi: Na John Gagarini, Kibaha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi