loader
Prince Charles alipokea £1M kutoka kwa familia ya Osama Bin Laden

Prince Charles alipokea £1M kutoka kwa familia ya Osama Bin Laden

MWANAMFALME wa Wales alikubali malipo ya £1m (Shilingi bilioni 2.847) kutoka kwa familia ya Osama Bin Laden, gazeti la Sunday Times limeripoti.

Prince Charles alikubali pesa hizo kutoka kwa kaka wa kambo wa Osama Bin Laden mwaka 2013, miaka miwili baada ya kiongozi huyo wa al-Qaeda kuuawa, taarifa hiyo imesema.

Mfuko wa Hisani wa Prince of Wales (PWCF) ulipokea mchango huo.

Clarence House ilisema ilikuwa imehakikishiwa na PWCF kwamba "uangalifu wa kina" umefanywa, na uamuzi wa kukubali pesa uko kwa wadhamini.

"Jaribio lolote la kuitambulisha vinginevyo ni uongo," iliambia BBC.

Clarence House pia ilisema ilipinga hoja kadhaa zilizotolewa katika makala ya gazeti hilo.
Bin Laden alikataliwa na familia yake mwaka 1994 na hakuna maoni kwamba ndugu zake wa kambo walikuwa na uhusiano na shughuli zake.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d7d7e7f5d8417919d354756f2749f3e0.JPG

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: BBC

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi