loader
Chongolo aonya siasa kwenye sensa

Chongolo aonya siasa kwenye sensa

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameonya wananchi na wanasiasa kuwa Sensa ya Watu na Makazi, sio jambo la kisiasa bali ni la maendeleo ya Watanzania wote, hivyo wajitokeze kuhesabiwa na kamwe wasikubali kuhusisha jambo hilo na siasa.

Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Kaloleni Wilaya ya Moshi Mjini, alipozungumza na wananchama wa CCM Shina namba mbili.

Akihamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi, inayofanyika Agosti 23, mwaka huu nchi nzima, Chongolo alisema sensa sio suala la kisiasa na kuonya wanaCCM  na wananchi wasikubali kuhadaiwa kuwa sensa ni suala la siasa.

"Niwaonye wana CCM na wananchi kwa ujumla, msikubali kudanganywa kuwa sensa ni suala la kisiasa hili sio kweli, sensa ni kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, serikali inapanga maendeleo kulingana na idadi ya watu kwenye maeneo yao, sasa msiposhiriki kikamilifu mtajikwamisha wenyewe,"amesema Chongolo.

Amesema sensa inafanywa ili kujua idadi ya watu katika maeneo yao, ili mipango ya maendeleo inapopangwa na serikali miradi ipelekwe kwenye maeneo husika, kulingana na idadi ya watu iliyopo.

"Asije mtu akakuambia sensa ya agenda ya chama fulani,hapana msikubali kudanganywa,sensa ni jambo linalofanywa na serikali la kitaifa kwa ajili ya maendeleo yao,"anasisitiza Chongolo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ef431924b3b32f15fe95b0e8678f0818.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Moshi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi