loader
36 wajitokeza ubunge EALA,

36 wajitokeza ubunge EALA,

MAKADA 36 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitosa kuwania ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) na kufanya chama hicho kuvuna shilingi milioni 36.

Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea nafasi hizo kupitia CCM umenza Agosti Mosi, mpaka leo Agosti 3, 2022 jumla ya wanachma 36 wamechukua fomu ambapo fomu moja ni shilingi milioni 1.

Makusanyo hayo ya fedha ni kutoka ofisi tatu za CCM ambazo ni Makao Makuu ya CCM - Dodoma, Afisi Kuu ya CCM - Zanzibar na Ofisi Ndogo ya CCM-Dar es Salaam

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni CCM, Solomoni Itunda  amesema kuwa wanachama  waliochukua fomu ni Francis Nanai, Pascal Mayala, Jonas Lufungulo, Dk Linda Salekwa, Loti Lembrice, Richard Mbuguni, Angela Kiza, Melinda Muganda, Fikiri Luganga, Mkondo Fabian, Albert Mbago, Robison Etuttu na David Mwakanjuki.

Wengine ni Amani Kajuna, Azizi Mussa, Judith Mollel, Amedeus Mzee, Kalunde Malale, William Reuben, Fancy Nkuhi, Khuni, Salma Mwassa, Ngwaru Maghembe, Happyness Lugiko, Shabu Makonyola, Salimu Kungulilo, Prof Norman Sigalla, Harrison Lukosi, Rehema Hassan, Ahmed Nkhuli, Steven Mkomwa, Dorica Gwilenza na Ansar Kachabwa.

Aliongeza kuwa wengine ni Nadra Juma Mohamed, Ahmed Shehe Saleh, Mar-yam Said Mussa na Mourie Oscar Sendera.

Itunda alitoa wito kwa wanachama wengine wenye vigezo kuendelea kujitokeza kuchukua fomu ii kuwania nafasi hizo ikiwa ni kutimiza takwa la kikatiba.Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 10, 2022

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/62017ded270a439a7fafee725c55fe69.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi