loader
Mpango apiga marufuku Rumbesa

Mpango apiga marufuku Rumbesa

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amepiga marufuku Halmashauri kutumia rumbesa kuwa chanzo cha mapato na badala yake ametaka mazoa ya kilimo na mifugo yapimwe kwenye mizani.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Agosti 3, 2022 imesema kuwa Dk Mpango ametaka wakuu wa mikoa na wa wilaya kuhakikisha mazao ya kilimo na mifugo inapimwa kwenye mizani.

"Rumbesa sasa hapana. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mhakikishe mazao ya viazi, mpunga, mahindi yauzwe kwa kupimwa kwenye mizani na hili lifanyike pia kwenye mifugo.” Amesema na kuongeza

" Na kwa Halmashauri faini za rumbesa isiwe chanzo cha mapato."

Aidha, Dk Mpango ameagiza  Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka mfumo ambao utawezesha Wizara za Kisekta kusimamia na kufuatilia utendaji wa wataalamu wa sekta zao ambao wako Halmashauri.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b689efdc06328a8d0e2b9bf277e4708f.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi