loader
Aliyeuwa mwanafunzi UDSM adakwa

Aliyeuwa mwanafunzi UDSM adakwa

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemtia mbaroni mtuhumiwa Gadi Daudi maarufu ‘Jeshi la Mtu mmoja’ (28) mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Julius Fredrick (22).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumn ya Dar es Salaam Muliro Jumanne amesema Gadi alimuua mwanafunzi huyo na kumpora simu yake ya mkononi.

“Tukio hilo lilitokea Julai 16, 2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.”Amesema Muliro

Amesema  Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina Julai 27, 2022  na lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza.

“Baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyang'anyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam,”amesema

Aidha, Muliro amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio ya kiuhalifu maeneo ya Mlimani City, Mwenge na Kawe na pia aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha kesi namba 256/2020 na kuhukumiwa kifungo cha  miaka 30 tangu Julai 6, 2020.

“Hata hivyo aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.”Amesema

Muliro amesema Agosti Mosi, 2022 majira ya saa kumi na nusu jioni mtuhumiwa huyo alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani City na Hostel za Magufuli.

“Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi. Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji .

Muliro amesema katika eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ff68bd1631102e0b966830259650c01e.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi