loader
Kopa kuachia EP hivi karibuni

Kopa kuachia EP hivi karibuni

MKALI wa muziki wa taarabu, Khadija Omar Kopa amewapasha mashabiki zake kuwa anatarajia kuachia EP yake itakayokuwa na ngoma tano.

Malkia huyo wa mipasho ambaye kwa muda mrefu hajasikika akitikisa kwenye muziki huo wenye asili ya Pwani, amewaeleza mashabiki hao kuwa wasimuone yuko kimya ila anajipanga kuwaletea burudani.

Ingawa hakuweka wazi juu ya lini ataachia EP hiyo au kudokeza maelezo mengi kuhusiana na hilo, lakini amewataka mashabiki wake waendelee kumvumilia kidogo kabla ya kuachia ngoma zake hizo.

“Mimi nipo, mashabiki wangu wasione nipo kimya, nimekuwa na shughuli zangu kama kawaida wavumilie kidogo, hivi karibuni nitaachia nyimbo zangu tano kwa pamoja, hivyo wasiwe na wasiwasi, nitawajuza vizuri kinachofuata,” alisema Kopa.

Mbali na hilo, Kopa pia alishukuru kujaliwa vipaji ndani ya familia yao akieleza kuwa hiyo ndiyo zawadi yao na wamekuwa wakiifanya sanaa hiyo kwa ushindani mkubwa kama ilivyo sasa kwa mwanawe wa kike, Zuhura Soud ‘Zuchu’ na marehemu Omar Kopa aliyekuwa akiimba taarabu pia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4ce7d21300169e861cbf86cdef9fd1bd.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi