loader
Duma mbioni kuachia filamu

Duma mbioni kuachia filamu

NYOTA wa filamu nchini, Daud Michael ‘Duma’ amesema yupo katika hatua za mwisho kuachia filamu yake mpya aliyoiandaa kwa gharama kubwa.

Akizungumza na HabariLEO, msanii huyo ameelezea namna mchakato wa kukamilisha filamu hiyo pamoja na wasanii aliowashirikisha.

“Ni filamu kubwa ambayo ina ubora wa hali ya juu kutokana na gharama nilizotumia, lakini ndani yake kuna mastaa wengi, ambao wameshiriki lengo langu ni kufikisha ujumbe na kuonesha ubunifu wa tofauti na kazi zangu nilizotoa huko nyuma,” alisema Duma.

Msanii huyo ameeleza kuwa mpango wake ni kuiachia filamu hiyo ifikapo Oktoba na amepanga kuitangaza ndani na nje ya Tanzania sababu kwa ubora wake anaamini utamtangaza vizuri.

Alisema lengo lake ni kutaka kujulikana kimataifa na kuingizwa kwenye kushindania tuzo mbalimbali za filamu duniani ili kujipatia tuzo.

Duma amewaomba mashabiki wake kumpa sapoti kwa kuhudhuria uzinduzi wa filamu hiyo ambayo jina lake atalitoa baada ya kuikamilisha pia ataweka hadharani majina ya watu maarufu ambao atawaalika kuhudhuria uzinduzi huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/388e0934f0c2129ac56664f11a34288e.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi