loader
Harmonize afurahia kutumbuiza Singida

Harmonize afurahia kutumbuiza Singida

MKURUGENZI wa lebo ya Konde Worldwide, Abdul Kahali ‘Harmonize’ amesema kuwa amefurahi baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Singida Big Stars, ni jambo la heshima kwake na mashabiki wasubiri kushuhudia historia ikiandikwa mkoani humo.

Harmonize atatumbuiza wakati Singida Big Stars, watakapokuwa wakiwatangaza wachezaji wao wapya na baadae kufuatiwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Alisema kuwa ni jambo kubwa kuaminiwa na timu ya Singida Big Stars, ambayo licha ya kuwepo wasanii wengi hapa nchini lakini wamempa yeye nafasi hiyo ya kutumbuiza na kusisitiza hawajakosea kufanya hivyo kwani anaenda kuandika historia ya mkoani Singida.

“Watu wangu wa Singida, kaeni tayari kwa onyesho la kihistoria, naamini hakuna mtu ambaye atajutia kuja kwenye siku hii ya Singida Big Stars, burudani itakayotolewa hapo ni ya viwango vya juu sana.”

“Sitaki kuwa muongeaji sana tukutane uwanjani tufurahie muziki mzuri na tuwashuhudie wachezaji wetu wapya huku tukiiunga mkono timu yetu ya nyumbani,” alisema Harmonize.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/64e9dd42f289da5ead96c830071c2220.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi