loader
Said Fella amsikitikia P Funk

Said Fella amsikitikia P Funk

MENEJA wa lebo ya WCB, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ amesema kuwa wamesikitishwa na kauli zinazotolewa na prodyuza mkongwe wa muziki hapa nchini, Paul Matthysse ‘P Funk’ kwamba wao wanawakandamiza wasanii.

Katika wiki mbili za karibuni, P Funk amekuwa akiijia juu lebo ya WCB, kuwa inawanyonya wasanii wake ndio maana wengine wameamua kujitoa ili kuanza maisha yao.

Hadi sasa wasanii waliokwisha ondoka kwenye lebo hiyo ni Raymond Mwakyusa ‘Ray Vanny’, Rajab Kahali ‘Harmonize’ na Richard Martin ‘Rich Mavoko’.

 Alisema kuwa ameshangazwa na maneno ya P Funk na huenda aliongea hayo akiwa ameweka vitu kichwani maana hawezi kusema tunaoongoza muziki ni mashehe watupu sio kweli muziki unaongozwa na kila mtu.

“Hadi anasema wananyonywa ni katika upande gani? Unasema wanaonewa kwenye nini katika mkataba wewe haupo sisi ndio tunaofanya hizo kazi unapata wapi nguvu ya kusema wananyonywa?”

“P Funk hajui chochote anakurupuka yeye alikuwa na wasanii wangapi? Profesa Jay ana malalamiko naye, Juma Nature japokuwa yeye huwa ni mtu wa kudharau, lakini kuna vitu vipo vilevile Ferooz yuko wapi? Solo Thang mpaka akaenda Uingereza,'' alisema Fella.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/91cb7c050e1c864331160f993524f18b.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi