loader
Mtanzania aboresha muda wake Madola

Mtanzania aboresha muda wake Madola

MWANARIADHA wa Tanzania, Joseph Panga ameweka muda wake bora mpya katika mbio za meta 10,000 katika Michezo ya 18 ya Jumuiya ya Madola inayoendelea mjini hapa.

Panga alimaliza wa nane kwa kutumia dakika 28:13:83 na kuupita ule wa awali kwa karibu sekunde 25 na kuweka muda wake bora binafsi. Muda wake bora wa awali ulikuwa dakika 28:38.

Mwanariadha huyo alimaliza katika nafasi ya nane huku Mganda, Jacob Kiplimo akitwaa dhahabu kwa kumaliza wa kwanza katika mbio hizo kwa kutumia dakika 27:09:19.

Ushindi huo wa Kiplimo unaendeleza umwamba mbele ya Wakenya baada ya wiki iliyopita, Mganda mwingine, Victor Kiplangat kushinda marathoni kwa kutumia saa 2:10:55, huku Mtanzania Alphonce Simbu akitwaa medali ya fedha kwa kutumia saa 2:12:29 na Mkenya, Michael Githae alitumia saa 2:13:16 katika nafasi ya tatu.

 Kiplimo, ambaye hivi karibuni alichukua medali ya shaba katika mashindano ya dunia ya riadha, juzi alishinda kwa kutumia dakika 27:09:19 na kumaliza mbele ya Wakenya Daniel Ebenyo na Kibiwott Kandie.

"Nafikiri kwangu kushinda Michezo ya Jumuiya ya Madola ni kila kitu na ndio kitu muhimu zaidi kwangu msimu huu,” alisema Kiplimo.

"Lakini bado kuna mambo mengi ya kufanya huko mbele katika Michezo ya Olimpiki na mashindano ya dunia.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9116d9df6d2399a8336d4839b58b6614.PNG

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: BIRMINGHAM, Uingereza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi