loader
Mil 58/- za M-BET zilivyotua kwa Mwaikimba

Mil 58/- za M-BET zilivyotua kwa Mwaikimba

MKAZI wa Mkoa wa Mbeya, Ojilloh Mwaikimba ameshinda Sh 58,650,180 baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia droo ya kampuni ya M-BET Tanzania.

Mwaikimba ambaye ni shabiki wa timu ya Manchester City alisema kuwa haikuwa rahisi kushinda fedha hizo kutokana na ugumu wa kubashiri mechi mbalimbali na hasa kipindi ambacho ligi zilikuwa zimesimama huku timu chache zikienda kufanya mazoezi ya kabla ya kuanza kwa msimu (Pre-season).

Alisema pamoja na changamoto hiyo, Mwaikimba ambaye ni mwalimu kitaaluma, aliweza kufanya ubashiri wake kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kupata fedha hizo.

Alifafanua kuwa alishinda fedha hizo wiki kadhaa zilizopita, lakini kutokana na tatizo la usajili wa simu yake hakuweza kupata fedha hizo katika muda huo kutokana na utaratibu wa kampuni ya M-BET.

Alifafanua kuwa alisajili laini yake ya simu kwa kutumia kitambulisho cha Taifa cha mtu mwingine, hali ambayo ilimfanya kuchelewa kupata fedha hizo.

“Jina langu halisi na lile la usajili lilikuwa tofauti na hivyo M-BET kushindwa kunilipa fedha kwani ingekuwa ni kinyume na taratibu. Ilinilazimu kuanza kufuata utaratibu wa usajili kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano na taratibu za M-BET na kulipwa fedha zangu.

“Nimeamini kuwa haki ya mtu haipotei kwani baada ya kushindwa kulipwa mara ya kwanza na kupewa utaratibu, nikawa na mawazo mengi sana kuhusiana na fedha hizo. Naishukuru M-BET Tanzania kwa kunikumbusha kuhusiana na kufuata taratibu za usajili wa laini za simu kwa majina sahihi na pia ninatoa wito kwa waliojisajili kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine, wafuate utaratibu,” alisema Mwaikimba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wataendelea kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na taratibu na kuwaomba watu wenye usajili tofauti na kitambulisho cha Taifa kufanya marekebisho.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fce6ec3355b5a37a234ee5c49a7aa9f2.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi