loader
Ngorongoro Half Marathon yamsapoti Samia

Ngorongoro Half Marathon yamsapoti Samia

MAANDALIZI ya msimu wa 14 wa Ngorongoro Half Marathon 2022 unaotarajia kufanyika Septemba 11 yanaendelea, huku lengo kuu likiwa ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Royal Tour.

Mkurugenzi wa mbio hiyo, Meta Petro alisema jana kuwa mbio ya mwaka huu ni maalumu kwa ajili ya kumuunga mkono Samia kuhusu filamu hiyo ya Royal Tour, ambayo inatangaza utalii wa Tanzania.

Rais Samia hivi karibuni alizindua filamu hiyo nchini Marekani kabla ya kuzinduliwa Arusha na baadae Dar es Salaam, Zanzibar na mikoa mingine.

Petro alisema kuwa mbio ya mwaka huu ni mahususi kuitangaza Royal Tour, ambayo inaendelea kuvuta watalii wengi kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.

Aliwataka watu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hiyo ya umbali wa kilometa 21, 10 na ile ya tano, ambayo kawaida huwa ya kujifurahisha.

Alisema kila mshiriki atatakiwa kulipia Sh 35,000 ili kupata namba ili kushiriki mbio husika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0fa4aa83f483340a2dc05be7ae98998a.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi