loader
Serengeti yawakabidhi Simba Queens mil 15/-

Serengeti yawakabidhi Simba Queens mil 15/-

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi ya Wanawake nchini maarufu Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite, imekabidhi zawadi ya hundi ya Sh milioni 15 kwa mabingwa wa ligi hiyo, Simba Queens.

SBL imetoa hundi hiyo siku chache baada ya ligi hiyo kumalizika kwa msimu wa 2021/2022.

Simba Queens waliibuka washindi kwa kuwafunga Mlandizi Queens mabao 2-1 na kukabidhiwa ubingwa ambao ni wa tatu mfululizo.

Tangu SBL iingie kama mdhamini mkuu kupitia bia ya Serengeti Lite, mvuto na ushindani vimekuwa vikiongezeka kwa kasi huku idadi ya timu ikiongezeka pia kutoka 12 mwaka 2018 hadi timu 18 sasa.

Mkurugenzi wa Sheria wa SBL, Lucia Minde, alisema muda mfupi baada ya kukabidhi hundi hiyo kuwa, udhamini huo umesaidia kuibua vipaji vya wanawake katika soka pamoja na timu zenye ushindani mkali zilizoitambulisha vyema ligi hiyo.

Kwa mujibu wa Lucia, Bia ya Serengeti Lite inajivunia kuwa mdhamini wa ligi hiyo na kwamba, udhamini huo umeongeza ushiriki wa wanawake kwenye michezo na hususani mpira wa miguu.

Alisema SBL kupitia Serengeti Lite inaamini kuwa, kutoa fursa kwa wanawake kuonesha vipaji vyao kwenye michezo kutasaidia kuwanyanyua na kuwezesha kuongeza vipato vyao kupitia michezo.

“Mpira wa miguu si tu burudani, bali pia shughuli ya kiuchumi ambayo imeajiri watu wengi duniani. Wanawake wanaoshiriki katika mchezo huu maarufu na wenye mashabiki wengi duniani wanajipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao,” anasema.

Kwa mujibu wa TFF, kipindi cha nyuma ilikuwa ni vigumu kwa timu kwenda kucheza mechi za ugenini kutokana na ukata, lakini kwa sasa hali imebadilika.

“Ilikuwa ni vigumu kwa timu kumudu gharama za usafiri, malazi na nyinginezo kwa ajili ya kucheza mechi za ugenini, lakini baada ya udhamini wa Serengeti Lite hili si tatizo kubwa tena,” alisema Lucia.

Udhamini wa Bia ya Serengeti Lite kwa ligi ya wanawake ni mwendelezo wa ufadhili kwa michezo unaofanywa na SBL kupitia bidhaa zake mbalimbali.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d66b6f7da1b38f0dfa530fbd95dfbb56.jpg

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi