MAHAKAMA ya Nairobi nchini Kenya imeiagiza tume huru ya uchaguzi na Mipaka nchini humo kutumia usajili wa daftari kuwatambua wapiga kura katika uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 9, 2020
Taarifa zilizopatikana nchini Kenya zinaeleza kuwa Mahakam hiyo pia ametupilia mbali barua ya IEBC ambayo waliiandikia Muungano wa Azimio, ikitaarifu kuwa watatumia vifaa vya kielektroniki vya kuwatanbua wapiga kura (KIEM).
Mahakama chini ya Jaji Mugure Thande, imetoa maamuzi hayo baada ya kugundua kuwa uamuzi uliopingwa wa Tume hiyo wa kutotumia daftari lililochapishwa unakiuka vipengee vilivyo wazi vya katiba ambayo inaeleza kuwa pale kifaa cha kielektroniki cha kutambua wapigakura kitafeli basi mpiga kura huyo atatambuliwa kwa kutumia sajili iliyochapishwa.
"Ni nini kitatokea kwa mpiga kura aliyesajiliwa ambaye maelezo yake hayawezi kuchukuliwa na kifaa cha KIEMs kwa kushindwa kwa teknolojia kwa kuzingatia uamuzi wa IEBC wa kutotumia rejista iliyochapishwa?" Mahakama ilihoji .
Jaji Mugure alisema ikiwa uamuzi huo utaruhusiwa kubaki bila kupingwa matokeo yatakuwa kwamba haki ya kikatiba ya wapiga kura ya kupiga kura chini ya Kifungu 38B itakiukwa.
Mgombea urais wa Azimio Raila Odinga mwezi uliopita alisisitiza msimamo wake wa kutumia usajili wa daftari yenye maelezo ya wapigakura