loader
CCM yataka maeneo huduma za kijamii yapimwe

CCM yataka maeneo huduma za kijamii yapimwe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzisha programu ya kutambua na kupima maeneo yote ya huduma za kijamii na kuyapa hatimiliki, ili kuepusha migogoro.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo mara baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mamsera Kati wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Chongolo yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku sita inayomalizika kesho, kukagua uhai wa chama, kuhamasisha wananchi kwenye sensa ya watu na makazi na kukagua utekelezaji wa ilani ya chama kwenye miradi ya maendeleo.

Amesema Tamisemi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wanapaswa kuwa na programu ya kutambua na kupima maeneo yote ya huduma za kijamii kama shule, hospitali, zahanati, viwanja vya huduma na kutoa hatimiliki, ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea.

"Lazima tuhakikishe maeneo yote ya huduma yanapimwa na kutolewa hati zihifadhiwe, ili kuepusha migogoro baadaye, Tamisemi na Wizara ya Ardhi lazima muweke programu za kutambua maeneo hayo nchi nzima yasije kuporwa,"amesema Chongolo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akizungumza mbele ya Chongolo, amewataka wananchi wa Rombo na mkoa huo kwa ujumla kudumisha usalama, amani na ulinzi na kuwahakikishia kuwa wananchi hao watafanya kazi zao kwa amani bila kuonewa au kuporwa mali zao.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d8dc0a18c9a1b9a3d266f91a93967711.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Rombo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi