loader
Rais Samia agomea ombi la Mbalizi kuwa Halmashauri

Rais Samia agomea ombi la Mbalizi kuwa Halmashauri

RAIS Samia Suluhu Hassan, amekataa ombi la wananchi wa mji wa Mbalizi, Mbeya vijijini la kuupandisha hadhi mji huo kuwa Halmashauri.

Rais Samia amesema kwa sasa kipaumbele chake ni kutatua shida za wananchi na si kuongeza gharama.

Rais Samia amekataa ombi hilo leo Agosti 5, 2022 akizungumza na wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya ambao walipaza sauti wakimtaka kuipandisha Mbalizi kuwa halmshauri ili kusogeza huduma za kijamii karibu.

Akijibu ombi hilo Rais Samia amesema, “Mbunge wenu (Oran Njeza) ameniambia lakini kuweka halmashauri maana yake ni gharama zaidi na nani anabeba ni serikali.”Amesema kwa kuhoji na  kuongeza  

“Jana nilipofika  uwanja wa ndege, Mkuu wa Mkoa na mbunge waliniambia kuhusu halmashauri lakini ndugu zangu, halmashauri maana yake ni viongozi zaidi, mishahara zaidi, magari zaidi, majengo zaidi, gharama kwa Serikali.”

“Kwa sasa hivi, wananchi wangu wa Tanzania wana shida chungu nzima, wanataka umeme, wanataka madarasa, wanataka huduma za afya. Mwaka jana tulijenga madarasa 15,000 sekondari na mengi katika shule za msingi.

“Lakini watoto wetu wanafanya mitihani karibuni hapa…mwakani natakiwa niwe na madarasa 8,000 Tanzania nzima. Yatabebwa na serikali ili msichangishwe, msibughudhiwe, serikali itafute hiyo pesa ikajenge madarasa….; “Bado mnataka vituo vya afya, mnataka maji. Tukisema tunakatana halmashauri, na Tanzania nzima inataka kukatwa maeneo, hatutaweza, uchumi wetu bado haujaruhusu. Acha tumalize shida za wananchi, tukishamaliza tutakwenda kukatana kwenye maeneo.” Amesema Rais Samia huku wananchi wakiitikia kwa sauti kubwa, … ‘Tumekuelewa mama’.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ecb0838024adcc0817d62ee9b1caed0d.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi