KATIBU Tawala (RAS) mpya Mkoa wa Mara, Msalika Robert Makungu amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Albert Gabriel Msovela leo 5 Julai, 2022.
Tukio hilo limefanyika kwenye jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika Ukumbi wa Uwekezaji, ambapo amezungumza na menejimenti pamoja na watumishi wa ofisi hiyo.
Hatua hiyo inafuatia mabadiliko ya hivi karibuni, ambayo yalifanywa na Rais Samia Suluhu Hassan yaliyomhamisha Msovela kutoka RAS wa Mara na kumpeleka kuwa RAS wa Kigoma.