loader
Rombo watakiwa kuombea amani uchaguzi Kenya

Rombo watakiwa kuombea amani uchaguzi Kenya

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amewaomba wananchi wa Rombo mkoani Kilimanjaro kuombea majirani zao wa Kenya, ili uchaguzi wao Agosti 9, mwaka huu ufanyike kwa amani.

Chongolo amesema uchaguzi huo ukifanywa kwa amani na utulivu,  utaifanya Wilaya ya Rombo na wananchi wake pia kuwa salama kwa sababu ni maeneo jirani na hali ikiwa mbaya, athari hutokea pande zote.

Kauli hiyo ameitoa leo akiwa Rombo, Tarakea kwenye shina la CCM Kikelelwa alipozindua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya chama hicho.

"Niwaombe kwanza hifadhini chakula, mvua hazikunyesha za kutosha, ukame ni mkubwa msiuze chakula. Lakini pia niwaombe waombeeni hao ndugu zenu, jirani zenu mwaka huu wana uchaguzi mkuu, ombeni ufanyike kwa amani na salama, usipokuwa salama na nyie hamtakuwa na amani tunategemeana," amesema Chongolo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5cc4daabf4367b9e6044029812036ceb.jpg

Tume Huru ya Uchaguzi na ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Rombo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi